James Kemoli Amata ni mwalimu mstaafu. Alifunza Kiswahili kwa miezi 376 katika Shule Kuu Sekondari ya Wasichana ya Moi, Eldoret (Septemba 1976 1986 na Julai 1990 Februari 2000); Shule ya Sekondari ya Wangulu, Wodanga (1987 Julai 1990) na Shule ya Sekondari ya ST John The Baptist, Likuyani (Februari 2000 2007) akastaafu.
Hivi sasa ni mwandishi asiye na mipaka huku akiwa mtekelezi wa tiba mbadala katika Kampuni ya Bidhaa za Afya ya Tiens na wakati uo huo akiwa mjasiriamali katika kampuni kuu ya Fountain Enterprises Progaramme (FEP).