Jack Na Shina la mharagweHapo zamani za kale, kulikuwa na kijana aliyeitwa Jack. Aliishi na mamake. Hawakuwa na pesa, lakini walikuwa na ng'ombe.Mamake Jack akasema, "Pesa zetu zimeisha. Nenda sokoni ujaribu kuuza ng'ombe yetu. Na ununue chakula na pesa utakayopata."