Rafiki, baadhi ya watu wamekuwa na ufahamu wa Mungu unaotokana na kuambiwa na watu wengine na sio kutoka katika neno lake [Biblia]. Njia ya kumfahamu Mungu kwa kutegemea watu zaidi na si neno lake ina madhara yake. Kama muelezeaji amemuelewa Mungu isivyo sahihi basi na wewe utamuelewa isivyo sahihi.
Neno "Mungu" [anaye abudiwa] ni cheo ambacho wanadamu wanatumia kumuelezea aliye mkuu kupita wote. Makao ya Mungu yako sehemu inaitwa mbinguni, lakini anakalia ulimwengu mzima pia.