Vita, vita na vita ni visa vya aibu. Binadamu hujidunisha kwa kupigana ovyoovyo. Tabia za uporaji na unyakuzi wa mali ya wengine ni unyama. Tabia ya kudai wageni wamechukua nafasi zetu ni upumbamvu na ukatili dhidi ya hadhi ya wanadamu. Tuwe watu, tukome kuwa viatu. Damu ya mtu huyu na ya mtu yule ni moja. Hapo aliye na damu ya kijani kiwiti. Kuwashawasha nyoto kukome tuishi kama ndugu na ndugu.