Mfalme Tunyelemumo anatangaza kuwa kiumbe chochote kitakachofanikisha kumpatia Tunda la mbuyu atakiozesha binti yake mzuwanda. Tangazo hilo linavivutia viumbe vingi. Wanajitokeza wanyama na binadamu kujaribu bahati. Kobe ambaye hakutarajiwa anajikuta anaipata bahati hiyo. Anafakiwa kuchuma tunda kileleni na kuozwa binti mfalme kwa shingo upande. Katika hali isiyotarajiwa, kobe anakuja kugeuka binadamu mtanashati chotara wa kiarabu na kiafrika, mtu anayeibuka ghalfa kuwa na ukwasi wa kupindukia.
CharlesJosephMloka ni mwandishi wa siku nyingi wa vitabu. Vitabu vyake vingine ni Diwani ya Mloka, Elimu Jamii na Chemsha Bongo, Lugha na Athari Zetu, Chaukaange, Pete ya Miujiza, The Wonderful Surgeon and Other Poems, Status, The Bush Rodent, The Parliamentary Privilege in Tanzania: Law and Practice, n.k. Mloka ana taaluma ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa ni mwandishi-mchapishaji, mhariri na mfasiri anayejitegemea.